HII KALI
NA JUMA NATURE ATIMULIWA EATV BAADA YA KUINGIA AMEVALIA KANDA MBILI NA KAUSHI
Msanii mkongwe na maarufu
nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature, ameonyesha kukerwa na kitendo
cha kutimuliwa jana usiku katika kipindi cha burudani cha televishen
inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa akifanya nao interview.
Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala na mara baada ya
mahojiano mafupi ya mwanzo mtangazaji alisema watarejea baada ya
mapumziko mafupi na ndipo Nature hakuonekana tena.
Kilichotokea kwa mujibu wa
Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko hayo, mtangazaji wa kipindi
hicho alimfuata na kumuambia kuwa hataendelea na interview tena kwasababu
ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha kukerwa
kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika yafuatayo kupitia ukurasa wake wa
facebook....
"hivi
kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha mahojiano
na kuvaa kaoshi ni tatizo....
kunywa nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na
hivi kama kweri we nimuandishi wa habari unaruhusiwa kuvaa vile kisheria
kama yule mtangazaji nimeboreka kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia
ssa kupeleka ngoma zangu pale siitaji interview"
AUNT EZEKIEL ALONGA "Wabunge wanataka kuniharibiha ndoa yangu
Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzi jijini Dar, Aunt alisema
waheshimiwa hao wanajua tayari yeye ameshaolewa lakini wamekuwa wakimpa
usumbufu mkubwa na kutoa ahadi balimbali, ndogo na kubwa kitendo ambacho
anaamini kinaweza kuhatarisha ndoa yake.
DIVA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameinua kinywa chake na kudai
kwamba kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kupata
penzi kwake, Amani linasimulia aliyoyasema
“Mimi nawashangaa sana baadhi ya waheshimiwa, wanajua tayari nimeolewa lakini wananitongoza, mimi siwezi,” alisema Aunt bila kuwataja majina wazito hao Akaongeza: “Mume wangu akisikia napata usumbufu kutoka kwa watu wazito, hawezi kuwa na amani, bado naipenda ndoa yangu na kuachana na Sunday wangu ni ndoto.”
Mwishoni mwa mwaka jana, Aunt alifunga ndoa na mfanyabiashara Sunday Dimonte, Dubai na mpaka sasa wanaishi kama mke na mume
ROSE NDAUKA ANASWA KIMAHABA ZAIDI
Staa
anayefanya poa katika sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amenaswa
akiwa kimahaba akifanya mambo ya chumbani hadharani na mchumba’ke,
Malick Bandawe, Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu, lilijiri
wikiendi katika Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo Coco Beach, Dar ambapo
kulikuwa na sherehe ya ‘bethidei’ ya mdogo wake Rose, Recho Ndauka.Baada
ya kukolea kwa ‘maji’,
Rose na mwandani wake walianza kugandana kama ruba huku
wakifanyiana vitendo vya
kimalavidavi.Wakati burudani zikiendelea
ukumbini hapo, wawili hao walijitenga pembeni na kuanza kumwagiana
mabusu mfululizo huku kila mmoja akijitahidi kuzionesha hisia za upendo
alizonazo kwa mwenzake, jambo lililowashangaza baadhi ya wageni
waalikwa.
“Makubwa haya! Sijawahi kumuona Rose akiwa kimalovee hivi
yaani leo ndiyo mara ya kwanza ila kwa upande mwingine wanaendana na
wanapendeza sema tu hawataki kufunga hiyo ndoa jamani tuione,” alisikika
dada mmoja akijadili na mwenzake.
Pamoja na hayo, sherehe hiyo ya
mdogo wake ilitawaliwa na vituko kibao baada ya wageni waalikwa kukolea
‘maji’ kwani kulikuwa na pombe kali tu huku wasichana wakiwa wamevalia
vimini vilivyoacha wazi sehemu kubwa za maungo nyeti hasa wakati
wakiserebuka hivyo
SITUMII KUNGU MANGA JAMANI HAYA NI MACHO YANGU ALISI(JACKLINE WOLPER)
No doubt that Jackline Wolper is one of the most sexiest actresses in
Swahiliwood hasa macho yake yakiwavutia fans wake wengi, hata hivyo
baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa Wolper anakula kungumanga ambazo
zinadaiwa kutumiwa na baadhi ya wanawake wa mjini ili wawe na macho
yenye mvuto,
hivyo Wolper pia anazila ili macho yake yalegee na kuwa na
mvuto wa kimahaba zaidi, huku wengine wakidai kuwa ni macho yake halisi
lakini huwa anayarembua na kuyalegeza kusudi ili aonekano ana mvuto
zaidi. kama kawaida Swahiliworldplanet ilimtafuta Wolper anayetamba
sokoni sasa na films kama Mr. Nobody, Curse of
Marriage na nyingnezo na
kumuuliza kuhusu issue ya kula kungumanga ili awe na sexy eyes, Wolper
alisema kuwa siyo kweli kuwa anakula kungumanga ili awe na sexy eyes
bali ndivyo alivyo na hata wadogo zake na aunt yake wako hivyo hivyo na
wamerithi kutoka katika familia yao upande wa kiume. alisema "hapana ni
macho yangu kwani hata wadogo zangu na ma aunt wapo hivyo hivyo kwa
kifupi ni my family upande wa kiume wapo hivyo". Angalia hapo chini
picha za macho ya Wolper anayodaiwa kuyalia kungumanga..........
No comments:
Post a Comment