Monday, 19 August 2013
Wednesday, 14 August 2013
ccm kagera yawafukuza madiwani wake 8 wa mani spaa ya mji wa bukoba
Bukoba: Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera kimewafukuza uanachama
wa chama hicho, madiwani wake wanane kutokana na kile kilichoelezwa kuwa
ni kukaidi maelekezo mbalimbali ya chama hicho, pia kushirikiana na
upinzani kukihujumu.
TIMU YA KASHAI YAFUDHU HATUA YA NUSU FAINALI KWA KUIFUNGA KAGONDO 3-1
Madiwani waliotimuliwa ni wale Manispaa ya Bukoba ambao wamekuwa
wakitajwa kumuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini ambaye pia ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ambaye amekuwa akivutana
vikali na Meya wa Manispaa hiyo, Anatory Amani.
Miongoni mwa waliotimuliwa ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba na
Diwani wa Kashai, Yusuph Ngaiza, aliyepata kuwa mbunge wa muda mrefu wa
Bukoba Mjini na baadaye Meya wa Manispaa hiyo, Samuel Ruhangisa ambaye
ni Diwani wa Kitendagulo na Diwani wa Buhembe, Alexander Ngalinda ambaye
pia alikuwa Naibu Meya.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Averin Mushi alisema uamuzi wa
kuwatimua madiwani hao umefikiwa jana na halmashauri ya CCM ya Mkoa kwa
kile alichosema ni kwa ajili ya “kulinda masilahi ya chama na wananchi
wa Bukoba”.
Ibara ya 93 (15) ya Katiba ya CCM inataja moja ya kazi za halmashauri ya
chama hicho ngazi ya mkoa kuwa ni: “Kumwachisha au kumfukuza uongozi
kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri ya
CCM ya Mkoa”.
Hata hivyo kipengele cha 14 cha ibara hiyo ya 93 kinasema hatua
kumwachisha au kumfukuza mtu uanachama itachukuliwa endapo halmashauri
itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za
uanachama.
Hatua ya kuwafukuza uanachama madiwani hao ambao pia watakuwa wamepoteza
nafasi zao za udiwani, imekuja siku chache tangu Mwenyekiti wa CCM,
Rais Jakaya Kikwete alipozitaka pande zinazohusika katika mgogoro huo
kumaliza kwa njia ya mazungumzo.
“Madiwani wote wa CCM walioendelea na mgomo hata baada ya maelekezo ya
Mheshimiwa Rais kwa kusaini barua ya kutaka Mkurugenzi aitishe kikao cha
kumwondoa Meya tumefikia uamuzi mgumu wa kuwafukuza uanachama kwa
masilahi ya chama na wananchi wa Bukoba,’’ alisema Mushi.
Mushi aliwataja madiwani wengine waliofukuzwa ni Robert Katunzi
(Hamugembe), Deus Mutakyahwa (Nyanga), Richard Gasper (Miembeni),
Mulungi Kichwabuta (Viti Maalumu) na Dauda Kalumuna aliyekuwa Diwani wa
Ijuganyondo.
Katibu huyo alisema Balozi Kagasheki na Meya Amani ambao mamlaka yao ya
uteuzi ni ya kitaifa na wanatakiwa kumaliza tofauti zao kama
walivyoelekezwa na Rais.
Mgogoro uliosababisha madiwani hao kutimuliwa uliibuka baada ya
Kagasheki kumtuhumu Meya Amani kwamba ameingiza Manispaa katika miradi
ya ufisadi hali ilioibua makundi na kukwamisha kufanyika hata vikao vya
Baraza la Madiwani.
Waliofukuzwa ni;
1.Richard Gaspar (Miembeni )
2.Murungi Kichwabuta (viti maalum)
3.Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)
4.Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)
5.Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)
6.Robert Katunzi (Hamugembe)
7.Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na
8.Dauda Kalumuna (ijuganyondo).
SOURCE:Chanel ten BUKOBA
NAPE ATOA TAMKO LA CCM NA UTARATIBU KUFUATIA MGOGORO WA MADIWANI 8 BUKOBA UAMUZI KUTOLEWA
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa tamko rasmi kuhusiana na mgogoro ambao
unaendelea hivi sasa katika Manispaa ya Bukoba ambapo Halmashauri Kuu ya
CCM ya Mkoa ilifikia uamuzi wa kuwafukuza madiwani wanane (8) katika
kikao Chake cha Jana tarehe 13/08/2013.
Kufuatia maamuzi hayo Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Ndugu Nape Nnauye ametoa tamko kuhusu utaratibu na Kanuni za Chama katika kufikia maamuzi hayo.
Ifuatayo ni Nukuu ya Tamko hilo:
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi wake wa kuwafutia dhamana ya CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba waliotokana na CCM.
Kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa mwisho. Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe.
Hivyo basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera.
Pamoja na hilo, tumepokea barua za Madiwani hao za kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa msingi wa madai ya kukiukwa kwa utaratibu katika kufikia uamuzi huo.
Tunawasihi wananchi wa Bukoba na Kata husika, wanachama na viongozi wote kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo suala hili linashughulikiwa na vikao vya Kitaifa.
Imetolewa na:-
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
14/08/2013

Shangwe za Wanyaluganda wa timu ya Kashai baada ya kufudhu hatua ya nusu fainali kwa kuifunga Kagondo 3-1
MICHUANO ya Kagasheki CUP 2013
Wachezaji wa Kashai wakipasha uwanjani
Mashabiki wakifurahia soka
Mchezaji Yusuph Kikoti
Kwa matokeo hayo timu ya kashai itakutana na timu ya Rwamishenye katika hatua inayofuata.
Tuesday, 13 August 2013
REDD'S MISS ILALA INA SOGEA HIVYO
Monday, 5 August 2013
MITINDO YA VITENGE
Hapana chezea lol
sometimes inabidi ushone kufuatana na muonekano wako unapendeza sana
pendeja toto langu la uhakika
Subscribe to:
Posts (Atom)