MGANGA AKUTWA NA KIGANJA CHA BINADAMU AKIMUUZIA MTEJA WAKE KWA MILIONI 100 HUKO MWANZA.
Mtu mmoja jijini Mwanza anadaiwa kukamatwa na kiganja cha mtu akiwa anajiandaa kumuuzia mteja kwa sh million 100.
Washukiwa walikamatwa jana karibia na uwanja wa ndege wa Mwanza wakifanya biashara hiyo haramu....
Baada ya upekuzi wa kina, mteja
alikuwa ana milioni 100 na mganga alikutwa na kiganja cha
binadamu ambacho kilikuwa kibichi kikitoa damu.
Kiganja hicho kilikuwa kimevishwa tunguri na nywele za binadamu.
RAY C ANARUDI KWA VISHINDO AMPA KIPIGO CHA MWAKA NORA KATIKA hali ya kushangaza, siku
chache baada ya kuripotiwa kupona na kuacha matumizi ya madawa ya
kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ anadaiwa kugeuka
mwanamasumbwi na kumpa kipigo mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’, Ijumaa
Wikienda limenyetishiwa.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio
hilo lilijiri wiki iliyopita ndani ya studio moja ya kurekodia muziki
iliyopo Kinondoni, Dar ambapo wawili hao walikutana walipokwenda
kurekodi ngoma zao.
Ilidaiwa kuwa akiwa studio hapo, Nora
alikutana na Ray C ambaye pia alizama mahali hapo bila mawasiliano na
prodyuza anayemtengenezea ngoma mpya.
Chanzo hicho kilipasha kuwa baada ya
Ray C kuingia studio hapo alimkuta prodyuza huyo akiandaa ngoma ya Nora
ambapo alihoji kilichompeleka mwigizaji huyo mahali hapo.
Ilidaiwa kuwa prodyuza huyo ambaye jina halikupatikana alimwambia Ray C kuwa Nora alifika kurekodi wimbo wake.
Ilisemekana kuwa Ray C hakuridhishwa
na majibu hayo, akaomba asikilizishwe ngoma hiyo ya Nora lakini baada ya
kusikiliza ilidaiwa kwamba Ray C aliiponda mbele ya Nora, jambo ambalo
mwigizaji huyo hakufurahishwa nalo.
Ilidaiwa kuwa Nora alipandwa hasira na kujikuta akimjibu mbovu Ray C.
Habari ziliendelea kutiririka kuwa
siku hiyo walimalizana kwa kusonyana na siku iliyofuta walikutana tena
studio hapo ambapo Ray C alidaiwa kutinga akiwa ‘masanga’.
Ilisemekana kuwa alipomuona Nora alianza kumpa vijembe, jambo lililosababisha Nora kushikwa hasira ndipo wakavaana na kuzichapa.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Ray C ndiye
aliyeibuka bingwa wa ndondi hizo kwa kumtwanga Nora hadi kumvimbisha
jicho kabla ya maprodyuza na watu wengine kufanya kazi ya ziada
kuwaamulia.
Ilisemekana kuwa baadaye Ray C
alitolewa nje ndipo akahamishia hasira kwenye gari la Nora aina ya
Toyota Vitz kisha akalivunja kioo na kutambaa zake.
Baada ya kupenyezewa ‘niuz’ hizo
gazeti hili lilimtafuta Nora ambaye alikiri kutokea kwa sekeseke hilo
huku akibainisha namna alivyoumizwa jicho lake na kuvunjiwa kioo cha
pembeni cha gari lake.
Aliongeza kuwa siku hiyo alipoteza pochi wakati wa ugovi huo.
“Ray C alinikuta studio nikifanya wimbo, kilichonishangaza baada ya kuniona tu alibadilika ghafla.
“Nilijua angenishauri kwa kuwa ndiyo ninaanza gemu kumbe mwenzangu alifikiria vingine,” alisema Nora na kuongeza:
“Mbali na kuniumiza jicho lakini
alinifanyia mambo ya ajabu sana, kama kusingekuwa na watu wa kutuamulia
basi chochote kingetokea.
“Sikwenda kuripoti polisi. Niliamua
kusamehe kwa sababu kuna watu walinisihi niachane naye kwa sababu bado
kuna mambo yanamwendesha.
Kwa upande wake Ray C alitafutwa kwa
kila njia kupitia simu ya mkononi na kumvizia studio lakini hakupatikana
hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.
No comments:
Post a Comment