BURUDANI NA MICHEZO

 HII  KALI
   NA  JUMA  NATURE  ATIMULIWA   EATV   BAADA YA  KUINGIA  AMEVALIA KANDA MBILI  NA  KAUSHI
Msanii mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature, ameonyesha kukerwa na kitendo  cha  kutimuliwa  jana usiku katika kipindi cha burudani cha televishen inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa akifanya nao interview. 
Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala na mara baada ya mahojiano mafupi ya mwanzo  mtangazaji alisema watarejea baada ya mapumziko mafupi  na ndipo Nature hakuonekana tena.
  Kilichotokea kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko hayo, mtangazaji wa kipindi hicho alimfuata na kumuambia kuwa hataendelea na interview tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika yafuatayo  kupitia ukurasa wake wa facebook....

"hivi kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha mahojiano na kuvaa kaoshi ni tatizo....

kunywa nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na hivi kama kweri we nimuandishi wa habari unaruhusiwa kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji nimeboreka kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa kupeleka ngoma zangu pale siitaji interview"
AUNT EZEKIEL   ALONGA "Wabunge  wanataka kuniharibiha   ndoa  yangu
 



























Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzi jijini Dar, Aunt alisema waheshimiwa hao wanajua tayari yeye ameshaolewa lakini wamekuwa wakimpa usumbufu mkubwa na kutoa ahadi balimbali, ndogo na kubwa kitendo ambacho anaamini kinaweza kuhatarisha ndoa yake.
DIVA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameinua kinywa chake na kudai kwamba kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kupata penzi kwake, Amani linasimulia aliyoyasema

 

“Mimi nawashangaa sana baadhi ya waheshimiwa, wanajua tayari nimeolewa lakini wananitongoza, mimi siwezi,” alisema Aunt bila kuwataja majina wazito hao Akaongeza: “Mume wangu akisikia napata usumbufu kutoka kwa watu wazito, hawezi kuwa na amani, bado naipenda ndoa yangu na kuachana na Sunday wangu ni ndoto.”
 Mwishoni mwa mwaka jana, Aunt alifunga ndoa na mfanyabiashara Sunday Dimonte, Dubai na mpaka sasa wanaishi kama mke na mume



 ROSE  NDAUKA ANASWA KIMAHABA  ZAIDI 


Staa anayefanya poa katika sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amenaswa akiwa kimahaba akifanya mambo ya chumbani hadharani na mchumba’ke, Malick Bandawe, Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu, lilijiri wikiendi katika Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo Coco Beach, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya ‘bethidei’ ya mdogo wake Rose, Recho Ndauka.Baada ya kukolea kwa ‘maji’,      Rose na mwandani wake walianza kugandana kama ruba huku wakifanyiana vitendo vya 
kimalavidavi.Wakati burudani zikiendelea ukumbini hapo, wawili hao walijitenga pembeni na kuanza kumwagiana mabusu mfululizo huku kila mmoja akijitahidi kuzionesha hisia za upendo alizonazo kwa mwenzake, jambo lililowashangaza baadhi ya wageni waalikwa.
“Makubwa haya! Sijawahi kumuona Rose akiwa kimalovee hivi yaani leo ndiyo mara ya kwanza ila kwa upande mwingine wanaendana na wanapendeza sema tu hawataki kufunga hiyo ndoa jamani tuione,” alisikika dada mmoja akijadili na mwenzake.
Pamoja na hayo, sherehe hiyo ya mdogo wake ilitawaliwa na vituko kibao baada ya wageni waalikwa kukolea ‘maji’ kwani kulikuwa na pombe kali tu huku wasichana wakiwa wamevalia vimini vilivyoacha wazi sehemu kubwa za maungo nyeti hasa wakati wakiserebuka hivyo

 

 

SITUMII  KUNGU  MANGA  JAMANI HAYA  NI MACHO YANGU         ALISI(JACKLINE WOLPER)

 

No doubt that Jackline Wolper is one of the most sexiest actresses in Swahiliwood hasa macho yake yakiwavutia fans wake wengi, hata hivyo baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa Wolper anakula kungumanga ambazo zinadaiwa kutumiwa na baadhi ya wanawake wa mjini ili wawe na macho yenye mvuto, 

hivyo Wolper pia anazila ili macho yake yalegee na kuwa na mvuto wa kimahaba zaidi, huku wengine wakidai kuwa ni macho yake halisi lakini huwa anayarembua na kuyalegeza kusudi ili aonekano ana mvuto zaidi. kama kawaida Swahiliworldplanet ilimtafuta Wolper anayetamba sokoni sasa na films kama Mr. Nobody, Curse of 

Marriage na nyingnezo na kumuuliza kuhusu issue ya kula kungumanga ili awe na sexy eyes, Wolper alisema kuwa siyo kweli kuwa anakula kungumanga ili awe na sexy eyes bali ndivyo alivyo na hata wadogo zake na aunt yake wako hivyo hivyo na wamerithi kutoka katika familia yao upande wa kiume. alisema "hapana ni macho yangu kwani hata wadogo zangu na ma aunt wapo hivyo hivyo kwa kifupi ni my family upande wa kiume wapo hivyo". Angalia hapo chini picha za macho ya Wolper anayodaiwa kuyalia kungumanga..........



No comments:

Post a Comment