Monday 18 November 2013

Wema Sepetu arudi kwenye mitandao ya kijamii kwa mara ya kwanza baada ya msiba.

 Wema Sepetu arudi kwenye mitandao ya kijamii kwa mara ya kwanza baada ya msiba.mitandao ya kijamii baada ya muda mrefu toka msiba wa baba yake ulipotokea hivi karibuni
Katika post hiyo Wema amewataka “Teamwema” wapunguze jazba juu yanayotokea juu yake na kuwasihi kuwa wapunguze kutumia lugha ya matusi kwenye mitandao hiyo maana wanamuumiza ‘madame’
Ujumbe wake unasomeka kama ifuatavyo….
"...my darlings... im still grieving... i know you guys miss me... nd i miss you more... im jus still nat okay... but im right here... nipo pamoja na nyinyi... muda tu kidogo... dats all im asking for... nawapenda... saana kupita maelezo... im gone be baq... very soon... i promise... its jus dat sipo sawa. .. but inshallah... ntakuwa sawa... inshallah... its hard... i hope mnanielewa... i repeat nawapenda mno... mno... more dan u think... u kip me goin... u make me who iam... sema tu msifanye vile basi... msitukane... me mwenzenu bado im nat okay... alafu mnaniongezea matatizo... mi spendi... all in all i still love you guys... basi msinikere... sawa... sometimes its best to jus keep quiet... okay.... much love... P.S: Iam a father's daughter
  
Mwanamuziki Linex Sunday kuonekana ndani ya filamu mpya ya aunty Ezekiel - 'Mwajuma'Mwanamuziki Linex Sunday kuonekana ndani ya filamu mpya ya aunty Ezekiel - 'Mwajuma'
Msanii Linex Sunday Mjeda aka The V.O.A ameamua kufungua ukurasa wa pili wa kipaji ambacho hajawahi kukionesha cha uigizaji, hivi karibuni ataonekana katika filamu mpya ya muigizaji wa bongo movie Aunty Ezekiel inayoitwa ‘MWAJUMA’.
Kwa mujibu wa tovuti ya bongo5, linex ameeleza kuwa  filamu ya Mwajuma inahusu mwanadada aliyekuwa na maisha ya chini akiwa mama ntilie na baadae kuja kufanikiwa na kuanza maisha ya kihuni hususani kubadilisha wanaume kama nguo
Filamu hii inatarajiwa kutoma mwishoni mwa mwezi ujao

Tazama mwonekano mpya wa Ray akiwa na staili mpya ya nywele na Tatoo mwilini

Tazama mwonekano mpya wa Ray akiwa na staili mpya ya nywele na Tatoo mwilini

 

Johari atimkia Canada, tetesi zadai amepata “mchuchu wa kizungu”, Uwoya ampa ujumbe mzito 

Mwanadada Johari chagula ametimka nchini jana kuelekea nchini Canada kwa shughuli zake binafsi amabzo bado hatujaweza kupata taarifa kamili mpaka sasa

Kwa mujibu wa picha tulizozipata kupitia kwa Irene Uwoya kwenye mitandao ya kijamii , mwanadada huyo inasemekana amepata mpenzi wa kizungu ambaye ndio amemualika huko nchini Canada.
Bado tunaendelea kutafuta ukweli hasa wa sababu ya safari yake hiyo na tutawajulisha mara tutakapokuwa na taarifa kamili.
Naye Irene Uwoya aliamua kuwavunja watu mbavu kwa kumpa Johari ujumbe huu kama ishara ya kumtakia kila la kheri huko aendako. Irene aliandika…
“Yan wewe nirafiki yangu kipenz...bahat haiji mara mbili....sasa ukifika canada usinisahau ....maisha ndohayo...wazungu hawatak uswahili tuliaaaa…”Blandina Chagula (Johari)

Johari, Mahinda wamwagiana MATUSI ya nguoni kisa penzi la RAY

Kambi mbili za wasanii wanaotamba katika tasnia ya filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ na Blandina Chagula ‘Johari’, zimetupiana matusi mazito.. 
 
Ruth Suka ‘Mainda’.
Chanzo cha yote ni Mainda kufunguka juu ya uhusiano wake na ‘kaka mkubwa’ katika tasnia ya filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na kufichua jinsi Johari na msanii mwingine, Chuchu Hans walivyomuingilia katika penzi hilo.
Mainda alimwaga ‘upupu’ Jumatano iliyopita na kumfanya kila shabiki wao awashwe na habari hiyo.













 SIKIA KEJELI ZA JOHARI
Mara baada ya kutoka kwa habari hiyo, Johari alinukuliwa na gazeti moja  akisema kwamba Mainda amembipu, atampigia akiashiria kwamba atajibu mashambulizi hayo.
Hata kabla ya kufanya hivyo, Johari aliwaambia waandishi wetu kwamba Mainda amewavua nguo na kuwaweka hadharani.
TIMU JOHARI
Kwa upande mwingine, baadhi ya wasanii wakubwa wanaoitumikia Kampuni ya Ray na Johari (RJ), kurekodi kazi zao, (Team Johari) wakamshambulia Mainda kwa matusi mazito kupitia mitandao ya kijamii kama vile Instagram na BBM.



 MAREKANI YAITAJA TANZANIA KUWA KINARA WA BIASHARA YA KUSAFIRISHA BINADAMU
 Dar es Salaam. Marekani imetoa ripoti inayozungumzia usafirishaji wa binadamu ya mwaka 2013, huku ikiitaja Tanzania kuwa kinara wa kunyanyasa wasichana, kuwatumikisha katika ngono na usafirishaji wa binadamu.

Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya nchi hiyo inayohusika na diplomasia (US Department of State, Diplomacy in Action), pia inaitaja Tanzania kuwa ni kitovu cha njia ya kusafirisha wanawake, watoto na wanaume ambao hutumikishwa kwenye kazi za mashambani na biashara ya ngono.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa Julai mwaka huu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Seneta John Kerry inaweka bayana kwamba biashara ya usafirishaji wa binadamu hufanywa na baadhi ya ndugu na marafiki ambao hutoa ahadi kwa wahusika kwamba wanakwenda kuwasomesha au kuwatafutia ajira nzuri mijini.



Unyonyaji wa wasichana wadogo na utumikishaji majumbani ndilo tatizo linaloongoza, ingawa kesi za watoto kusafirishwa kwa ajili ya biashara ya ngono katika mpaka wa Tanzania na Kenya zinaongezeka. Pia, wasichana wananyonywa kwenye maeneo ya utalii,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.



Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watoto kutoka Burundi na Kenya, watu wazima kutoka Bangladesh, Nepal, Yemen na India wanatumikishwa kufanya kazi kwenye sekta za kilimo, madini na majumbani nchini Tanzania.



Baadhi ya raia kutoka nchi jirani huingia Tanzania kwa hiari yao, lakini hulazimishwa kufanya kazi majumbani kabla ya kupelekwa kutumikishwa kwenye biashara ya ngono Afrika Kusini, Ulaya na Mashariki ya Kati,” inaeleza.



Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alimtaka mwandishi kumtumia ripoti hiyo kwa njia ya baruapepe ili aweze kuisoma na kuitolea maelezo.



Alipotafutwa siku ya pili, alisema kuwa ameipokea na kuikabidhi ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) ili ifanyiwe kazi na baadaye kutoa majibu.



“Ripoti niliipata nikaikabidhi ofisi ya DPP kwa kuwa wao ndio wanaoweza kuitolea maelezo baada ya kuisoma. Maoni yangu lazima yawe ya kitaalamu siwezi kusema bila kupata taarifa kutoka kwao,” alisema.



Lawama kwa Serikali



Ripoti hiyo inaitupia lawama Tanzania kwa kutokuwa na sheria thabiti za kupambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu, huku ikitolea mfano namna ilivyoshindwa kuwasaidia raia wake waliokuwa wakinyanyaswa nje ya nchi.



“Kamati ya Serikali ya kupambana na usafirishaji binadamu, haijachukua hatua za kutosha katika kutekeleza mpango mkakati wa kupambana na vitendo hivyo,” inaeleza na kuongeza:



“Serikali imeshindwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa usafirishaji wa binadamu kama ambavyo inaelekezwa kwenye sheria ya kudhibiti biashara hiyo ya 2008.”



Taarifa hiyo inaitaka Tanzania kuongeza nguvu katika kutekeleza sheria ya kudhibiti biashara ya kusafirisha binadamu ya 2008 kwa kuwakamata na kuwashtaki wahusika wote, lakini ikaikosoa kwa kusema inatoa adhabu ndogo kwa mtu anayebainika kufanya makosa, ikiwa ni pamoja na kumhukumu kwenda jela miaka 10, kulipa faini au vyote viwili kwa pamoja.



“Sheria hiyo haifanani na nyingine kama za mtu anayepatikana na kosa la kubaka au kufanya kosa jingine la jinai. Mamlaka imesema ina kesi nne inazozichunguza, saba zipo mahakamani toka mwaka jana, zikiwepo mbili mpya,” inasema ripoti.



Pia, Serikali ya Tanzania imelaumiwa kwa kushindwa kuripoti maendeleo ya uchunguzi wa maofisa wake waliotuhumiwa kujihusisha na biashara ya usafirishaji binadamu.



LHRC na TGNP



Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema tatizo la usafirishaji wa binadamu pia linachangiwa na wasichana kuwa na tamaa ya maisha mazuri, hivyo kukubali ahadi ambazo hupewa kwamba wanapelekwa kusoma, wasifahamu wanarubuniwa.



“Wengi wanatamani kwenda ‘majuu’ wakidhani watapata elimu, lakini baadaye wanaingizwa kwenye vitendo vinavyowafedhehesha na kuwafanya wakate tamaa kabisa,” alisema.



Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya alisema katika siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wasichana waliochukuliwa vijijini kwenda mijini kufanya kazi.



Alisema pamoja na tatizo hilo kuongezeka hapa nchini, hakuna tafiti za kutosha ambazo zimefanywa na wadau mbalimbali kuonyesha madhara yaliyopatikana hadi sasa.



“Katika siku za usoni kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya kunyimwa chakula, kupigwa na kufukuzwa kazi huku wasichana wengine wakitumika kwenye biashara ya ngono,” alisema na kuongeza:



“Ripoti hii isiishie kwenye makabrasha bali ifanyiwe kazi ili jamii yote ijue kuwa hili ni tatizo.”



Ripoti hiyo inabainisha kuwa watu 47,000 pekee ndio walioweza kuokolewa mwaka jana kutoka kwenye mazingira ya utumikishwaji kati ya milioni 27 waliopo katika hali hiyo duniani.


Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi 44 ambazo zinajaribu kupambana na biashara hiyo, lakini hali inazidi kuwa mbaya zaidi

 




  

Monday 4 November 2013

P.SQUARE WAMEWEKA FURNITURE ZA DHAHABU NYUMBANI KWAO

4eb1c8da43d911e3bc6522000ae91414_8Wanandugu wawili ambao ni mapacha Peter Okoye na Paul Okoye, leo hii wameushangaza ulimwengu mara baada ya picha zao wakiwa kwenye sebule na dinning room iliyonakshiwa na dhahabu kwenye samani zake kuzagaa mitandaoni huku zikisindikizwa na maneno yenye kujiamini ndani yake.
7493d06843dc11e3a21b22000ae913ab_8
8300d71043da11e399e522000a9e28c4_8
3799cde443d611e3be7422000a9e0172_8
Kama kweli mng’o unaoonekana kwenye vitu hivi vyote ni dhahabu, basi hakuna sababu kuna kila sababu ya kuwaita wafalme wa mziki Africa kutokana na thamani ya pesa waliyotumia kutengeneza samani hizi.

Friday 1 November 2013

Diamond awapa "makavu" wanafiki wa Wema Sepetu. Soma hapa alichokiandika


"Mwenyez mungu alituagiza kuzika na ndiomaana leo tuko hapa... na sio kwenda sehem uliyokuwa unaforce wewe ili kesho upate picha za kuzusha instagram...! Upo...? Nakwambia, wewe ulokuwa unaandika upuuzi kwenye Comment..."
Hayo ni maneno ya Diamond Platnumz kwa wanafiki wa kipenzi chake na rafiki yake Wema Sepetu walihudhuria msiba kwa malengo tofauti na ya kumfariji dada yetu dada aliyepata msiba wa kuondokewa na baba yake mzazi hivi karibuni.
 
Baada Ya Miezi Michache Ndani Ya Ndoa Bob Junior Aachana Na Mke Wake, Fuatilia HapaMsanii Bob Junior amefunguka leo kupitia sammisago.com kuwa yuko single baada ya ndoa yake kuvunjika mwezi moja uliopita. Wasanii wengi huwa wanapata wakati mgumu wanapo funga ndo kwa sababu ya umaarufu na ratiba za maisha yao kabla ya kufunga ndoa.
Bob Junior leo mchana ametambulisha wimbo wake mpya na kutoa taarifa kwa mabinti wote kuwa kwa sasa Bob Junior ni single boy kumanisha kuwa ameachana na mke wake mwezi moja uliopita.  Kuogopa kuweka mambo ya familia waze Bob Junior hajasema haswa Sababu ya kuachana na mke wake ila ameniambia kilicho changia ndoa yake kuvunjika ni Wivu wa mke wake.
 Bob Junior 1Bob junior ameniambia kuwa wivu ni moja ya sababu zilizofanya ndoa yake kuvunjika na kwamba  alikuwa na wakati mgumu sana kumuonyesha mke wake kuwa yeye ni muaminifu kutokana na kuwa star na kupendwa na mashabiki wa Kike.

Fahamu kuwa ndoa ya Bob Junior Imedumu kwa Mwaka Moja Na miezi 2 tu.

Ladies Bob Junior Is Available. lol

Range Rover yangu na mali zangu "sijahongwa" nimenunua kwa pesa zangu - Irene Uwoya


Baada ya fans wengi kuanza “kumponda” mwanadada Irene Uwoya kuwa gari aina ya Range Rover aliyoinunua “amehongwa na washika dau”, mwanadada huyo ameibuka na  kusema kuwa mali anazomiliki amezinunua kwa pesa zake anazopata kwenye uigizaji  pamoja na zile zinazotokana na biashara zake nyingine.
 “Kwa nini watu hawataki kukubali kuwa kazi ya uigizaji inalipa, yaani sisi tukinunua magari tumehongwa? Yaani wa kuhongwa ni sisi tu na si tasnia nyingine?” alihoji Uwoya.
Aidha Uwoya alisema kuwa kazi ya filamu ukijua kuitumia vizuri kwa kujiwekea malengo na kuitumia vizuri kila senti unayoipata, unaweza kupata mafanikio makubwa.
“Tunaigiza sehemu nyingine ambazo hutaki hata mwanao aone, hii siyo kazi rahisi maana yake ni kwamba kama ukiipatia unaweza kujikuta unaingiza pesa kila siku kwani mwaka mzima uko kazini,” alisema
Irene amesema kuwa ameamua kuweka wazi ukweli huo kutokana na maneno yaliyozagaa kuwa magari anayomiliki amenunuliwa na wanaume ‘wanaomweka mjini’

Picha za mazishi ya Baba yake na Wema Sepetu yalivyokuwa leo huko Zanzibar.