Friday, 1 November 2013

Range Rover yangu na mali zangu "sijahongwa" nimenunua kwa pesa zangu - Irene Uwoya


Baada ya fans wengi kuanza “kumponda” mwanadada Irene Uwoya kuwa gari aina ya Range Rover aliyoinunua “amehongwa na washika dau”, mwanadada huyo ameibuka na  kusema kuwa mali anazomiliki amezinunua kwa pesa zake anazopata kwenye uigizaji  pamoja na zile zinazotokana na biashara zake nyingine.
 “Kwa nini watu hawataki kukubali kuwa kazi ya uigizaji inalipa, yaani sisi tukinunua magari tumehongwa? Yaani wa kuhongwa ni sisi tu na si tasnia nyingine?” alihoji Uwoya.
Aidha Uwoya alisema kuwa kazi ya filamu ukijua kuitumia vizuri kwa kujiwekea malengo na kuitumia vizuri kila senti unayoipata, unaweza kupata mafanikio makubwa.
“Tunaigiza sehemu nyingine ambazo hutaki hata mwanao aone, hii siyo kazi rahisi maana yake ni kwamba kama ukiipatia unaweza kujikuta unaingiza pesa kila siku kwani mwaka mzima uko kazini,” alisema
Irene amesema kuwa ameamua kuweka wazi ukweli huo kutokana na maneno yaliyozagaa kuwa magari anayomiliki amenunuliwa na wanaume ‘wanaomweka mjini’

Picha za mazishi ya Baba yake na Wema Sepetu yalivyokuwa leo huko Zanzibar.

No comments:

Post a Comment